JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
(IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII)
(IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KAULIMBIU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA
AFRIKA JUNI 16, 2017
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kwa kushirikiana na asasi za kiraia itaungana na mataifa mengine barani
Afrika kusherehekea sikuu ya mtoto wa Afrika kwa Mwaka 2017 Kitaifa mkoani
Dodoma tarehe 16 Juni mwaka huu.
Wizara inatoa taarifa kwa vyombo vya habari pamoja na
wadau wengine kuwa, Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa
mwaka huu 2017 ni “Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na
Fursa sawa kwa Watoto”.
Wizara inatoa wito kwa vyombo vya
habari waandishi wa habari kushirikiana na Serikali na wadau wengine katika kuelimisha
jamii kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu ambayo inahimiza uzingatiaji wa jukumu la ulinzi na
usalama wa Mtoto na utoaji wa haki sawa kwa watoto wote ili kufikia Malengo ya
Maendeleo Endelevu ifikapo mwaka 2030.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii)
06/6/2017
0 comments:
Post a Comment