Baadhi ya Wajumbe walioshiriki mafunzo ya Mkakati wa Kitaifa Kukomesha ukatili
wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto leo mjini Morogoro wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo leo jijini Morogoro
Wanawake
na watoto nchini Tanzania wamekuwa wakifanyiwa
ukatili kwa kisingizio cha mila na desturi huku jamii ikishuhudia au
kusikia wanawake na watoto wakipigwa na wakati mwingine kubakwa na hata kuuwawa
na watu wa karibu ikiwemo waume au wapenzi wao.
Utafiti
wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2016 unaweka bayana kuwa Nchi za Afrika zilizochini ya Jangwa la
Sahara zinaingia hasara ya dolla billion 95 sawa na shilingi trilioni 212 kila
mwaka kutokana na kukosa usawa wa kijinsia na
kuendelea kuwepo kwa vitendo vya
ukatili wa kijinsia. Hali hii ni
ushahidi tosha kuwa vitendo vya ukatili vina madhara makubwa kwa maendeleo ya
nchi yetu.
Amesema
hayo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
ya Jinsia Bw.Julius Mbilinyi wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto - Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii Bibi Sihaba Nkinga wakati wa ufunguzi wa Mafunzo Kuhusu Mpango Kazi wa Taifa
wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto, kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Asasi za Kiraia leo Mjini Morogoro.
Bw.
Mbilinyi ameongeza kuwa tafiti
mbalimbali ikiwemo Taarifa kuhusu Idadi ya Watu na Afya wa mwaka
2015-2016 inaonesha kuwa idadi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa
nchini bado ipo juu ambapoTaarifa hii inaonesha kuwa “wanawake 4 kati ya 10
wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.
Aidha
Ukatili wa kimwili unaongezeka kadri umri unavyoongezeka na Asilimia 22 ya
wanawake wenye umri wa miaka 15-19 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili,
ukilinganisha na asilimia 48 ya wanawake wenye umri wa miaka 40-49”.
Aliongeza
kuwa madhara ya vitendo vya ubaguzi, unyanyasaji
na ukatili dhidi ya wanawake na watoto vimeathiri na vinaendelea kuwaathiri
kiafya, kisaikolojia na kijamii wahanga wa vitendo hivi. Hali hiyo pia
inaathiri ushiriki wao katika shughuli za kijamii, kiuchumi, kisiasa na
maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.
Aidha
katika kukabiliana na changamoto ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Wizara kwa kushirikiana na wadau
imefanya juhudi mbalimbali ikiwemo kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza
Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ambao utekelezaji wake utaanza Mwezi Julai,
2017 hadi Juni, 2022.
Amesema
kuwa mafunzo haya yameandaliwa ili kuhakikisha kuwa Mpango Kazi huu unaeleweka
na kutekelezwa ipaswavyo na wadau na Wizara imekuwa ikitoa mafunzo kuhusu
Mpango huu kwa wadau mbalimbali na mafunzo haya ya siku mbili yameandaliwa kwa ajili ya Maafisa Maendeleo ya Jamii wa
Mikoa ambayo haikupata nafasi ya kushiriki katika mafunzo yaliyofanyika Mwezi
Machi, 2017
|
0 comments:
Post a Comment