Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawasilisha mada katika Kongamano la Kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).
NA
ANTHONY ISHENGOMA- WIZARA YA AFYA
Uamuzi wa Serikali ya
Awamu ya Tano wa kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari
umewanufaisha wanafunzi wa kike ambao walikuwa wanakosa fursa hiyo kwasababu
baadhi ya wazazi walikuwa wanatoa kipaumbele kwa watoto wa kiume.
Hayo yamesemwa na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati
akifungua Kongomano la kwanza la Kimataifa la Kijinsia la Chuo Kikuu cha Elimu
Dar es Salaam (DUCE) alipomwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
Jijini Dar es Saalam.
Waziri Ummy amewataka
baadhi ya wananchi kutobeza uamuzi huo kwani unatoa fursa zaidi kwa mtoto wa
kike kunufaika na elimu tofauti na awali ambapo baadhi ya familia kwasababu ya
umasikini zilitoa kipaumbele kwa mtoto
wa kiume.
Aliongeza kuwa kuna
madai yakuongezeka kwa idadi ya wanafunzi akisema ongezeko hilo limetokana na
kuwepo kwa fursa ya elimu bure ambayo imewezesha watoto walikuwa wanabaki nyum
bani kutokana na umasikini kufaidika na uamzi wa serikali ya wamu ya tano kutoa
elimu bure.
Amekitaka Chuo Kikuu
kishiriki DUCE kufanya utafiti ili kujua watoto hawa waliosababisha ongezeko
hilo wanatoka familia za aina gani ili kuiwezesha serikali kuweka mipango
endelevu ya utoaji elimu hususani kwa watoto wanaotoka kaya masikini.
Aidha Waziri kuna
baadhi ya watu bado wanadhani wazo la kuwarejesha watoto wakike shuleni baada
ya kujifungua ni kuhamasisha uhuni akisema lengo la serikali ni kumsomesha
mtoto wa kike bila kujali mazingira yanayomzunguka kwasababu watoto wakike
kutoka familia tajiri wanapopata ujauzito uhamishiwa na shule binafsi na
kuendelea na masomo tofauti na mwanafunzi wakike kutoka kaya masikini.
Amekipongeza chuo
kikuu cha Dar es Salaam kwa kudahili wanafunzi wakike kwa asilimia 38 akiwataka
kufikia 50 kwa 50 ifikapo 2025 na kuhimiza watoto wakike kushiriki katika
masomo ya sayansi kwani takwimu zinaonesha udahili katika masomo ya sayansi
katika elimu ya juu bado yako chini ukilinganisha na wanaume.
Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Pofesa Rwekaza Mukandala wakati akitoa hotuba yake kwa
mgeni rasmi amesema kuwa tatizo la unyanyasaji na ukosefu wa fursa sawa
kijinsia ni tatizo la kihistoria duniani kote na kusema kuwa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam kitaendelea kufanya tafiti na kutoa elimu ya masuala ya kijinsia ili
kukabiliana na tatizo hilo ambalo limekuwepo kwa muda mrefu.
Naye Mkuu wa Chuo
Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) Profesa William Anangisye amesema tangu
kuanzishwa kwa DUCE zimekuwepo juhudi mbalimbali za kuwatafuta wanazuoni kutoka
nchi mbalimbali kufika chuoni hapo ili waweze kufundisha na kuzungumzia masuala
mbalimbali ya elimu ya kijinsia na usawa katika elimu ya juu.
Amewaambia washiriki
kongomano hilo lasiku mbili kuwa kuna washiriki kutoka zaidi ya nchi ishirini
na tano na linalenga kutoa matokeo ya tafiti mbalimbali za elimu ya kijinsia
kwa jamii na kutoa fursa muhimu miongoni mwa wanazuoni kujadili matokeo ya
tafiti hizo.
|
0 comments:
Post a Comment