Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Njinsia, Wazee na Watoto akiongea na
wajumbe wa ujumbe wa jimbo la Eastern Cape hawapo pichani kutoka Afrika Kusini
leo ofisini kwake. |
Ujumbe kutoka kutoka jimbo la Eastern Cape kutoka nchini
Afrika ya Kusini uko Nchini kwa ajili ya kujifunza kutoka Tanzania namna bora
ya fursa za kiuchumi kwa wanawake nchini, uwezeshaji wa wanawake na uendeshaji
wa Benki ya Wanawake Nchini.
Akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kiongozi wa Msafara wa ujumbe
toka Afrika Kusini Mhe. Nancy Sihiwaji Mbunge wa Jimbo la Eastern Cape amesema
ziara yaoa inatokana na utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa Wanawake Afrika
uliofanyika Nchini Afrika ya kusikini kuhusu uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Aidha ujumbe huu umetambelea Wizara hii ili kujifunza na
kupata uzoefu kutoka Nchini ni kuona ni jinsi gani Tanzania kwa kushirikiana na
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Njinsia, Wazee na Watoto wameweza kuanzisha
na kufungua Benki inayolenga kuwainua wanawake kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment