Friday, 8 July 2016



TANGAZO KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs)

Kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Baraza la Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali , Tangazo la Serikali Na. 95/2016, Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inapenda kuyajulisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwa kutakuwa na uchaguzi wa viongozi na wajumbe wa Baraza kutokana na Baraza la sasa kumaliza muda wake. Kwa tangazo hili wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyosajiliwa wanatakiwa kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi huu utakaofanyika kama ifuatavyo:

1.   Ngazi ya Wilaya tarehe 11 Agosti, 2016.
2.   Ngazi ya Mkoa tarehe 17 Agosti, 2016.
3.   Ngazi ya Taifa tarehe 23 Agosti, 2016.

Maelekezo mengine kuhusu uchaguzi tajwa yatatolewa na wasimamizi wa uchaguzi wa ngazi husika.

Imetolewa kwa niaba ya Kamati Tendaji leo 8 Mwezi Julai, 2016.



Ismail A. Suleiman
KATIBU MKUU

BARAZA LA TAIFA LA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NaCoNGO)

0 comments:

Post a Comment