Tuesday, 28 June 2016

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Bibi Sihaba Nkinga akifungua Mkutano wa watumishi wa Wizara (hawapo pichani) walioshiriki kikao kazi cha watumishi wote katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Wiki ya Utumishi wa Umma katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Raslimaliwatu Erasmus T. Rugarabamu na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE wa Tawi Edwin B. Mtembei. (Tarehe 24/6/2016). 
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, wakifuatilia kwa makini maelezo ya Viongozi wa Wizara ya Afya (hayapo pichani) wakati wa kipindi cha maswali na majibu kama sehemu ya kukuza democrasia na ushirikishaji wa wafanyakazi mahala pa kazi. Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii.(Tarehe 24/6/2016).

Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, wakifuatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mkuu wa Wizara, Bibi Sihaba Nkinga (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Watumishi wa Wizara uliofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii.(Tarehe 24/6/2016). 

1 comment: