TAARIFA
KWA UMMA
TUHUMA
KUHUSU NGOs KUHAMASISHA VITENDO VYA USHOGA
Siku za hivi karibuni
kumekuwepo na tuhuma za kuwepo kwa baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
(NGOs) yanayojihusisha na kuhamasisha vitendo vya ushoga nchini. Tunapenda
kuujulisha umma kuwa NGOs zinasajiliwa kutekeleza majukumu yanayokubalika
kisheria na kwamba vitendo vya kuhamasisha ushoga si majukumu halali yanayopaswa
kutekelezwa na NGOs. Tunazitaka NGOs kutekeleza majukumu yaliyo ndani ya
usajili wao na kuepuka vitendo vya uvunjifu wa sheria. Aidha, tunazidi
kusisitiza kuwa vitendo vya ushoga havikubaliki nchini kwani ni kinyume na
mila, desturi na sheria za nchi. Ofisi ya Msajili inaomba wadau na umma kwa
ujumla kutoa taarifa zitakazowezesha kuthibitisha tuhuma tajwa ili hatua stahiki
dhidi ya NGOs husika zichukuliwe. Taarifa zinaweza kutolewa kupitia namba
zifuatazo: 022 2110714/0222123143/ 0754391942/0715391942.
M.S.Katemba
MSAJILI
WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
01
Agosti, 2016
0 comments:
Post a Comment