WIZARA YA AFYA,
MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE
NA WATOTO YALAANI YUKIO LA KUNAJISIWA NA KUUAWA KWA MTOTO WA UMRI WA MIAKA TISA
(9) MKAZI WA KIJIJI CHA KAPANGA, WILAYANI SUMBAWANGA
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na watoto inalaani vikali tukio La mauaji ya mtoto wa kike, umri miaka 9,
ambaye alininajisiwa kwa zamu na watu wasiojulikana, na hatimaye kumkata
mapanga yaliyosababisha kuuawa kwa mtoto huyo mdogo, katika kijiji cha Kapanga,
wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Wizara imepokea kwa huzuni kubwa taarifa kuhusu mazingira ya mauaji ya
mtoto huyo, ambaye alifanyiwa ukatili mkubwa yaliyosababisha kifo cha mtoto huyo
katika umri mdogo.
Wizara inapongeza agizo la Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda, Paza Mwamlima, ambaye amelitaka jeshi la polisi wilayani Sumbawanga
kuhakikisha wanawasaka na kuwatia mbaroni watuhumiwa wa mauaji ya mtoto ili
hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika, na hivyo kuwa fundisho
kwa watu wengine.
Wizara inapongeza ushirikiano uliooneshwa na wakazi wa kijiji cha Kapanga
wilayani Sumbawanga, katika kumtafuta mtoto toka mafichoni kwa ajili ya kuokoa uhai
wake. Jitihada zilizofanywa na jamii ya Kapanga ni uthibitisho kuwa, ulinzi wa mtoto ni jukumu la wazazi, walezi na watu
wote katika jamii.
Kwa niaba ya Wizara ya
Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, tunatoa pole kwa marafiki
wa mtoto, wazazi, ndugu na majirani na familia kwa ujumla, na tunawaomba kuwa na
moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa.
Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

0 comments:
Post a Comment