Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, S. Nkinga akiwa na wajumbe wa Baraza la Watoto
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa
Baraza. Watatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa Baraza, Ameir Haji Khamis pamoja
na wajumbe wengine.Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa Msimbazi Center,
Jijini Dar es salaam, kuanzia tarehe 27- 29,Aprili, 2016
Katika kikao
cha Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tuliweza kukutana na mtoto
Getrude Clemency mkazi wa mkoani Mwanza, ambaye hivi karibuni aliwakilisha Tanzania
kwenye Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa lililofanyika New York Marekani. Wakati
akihojiwa na BBC Getrude aliweza kuongea maneno yafuatayo kuhusu uwakilishi
wake, shughuli anazofanya na Agenda aliyowasilisha katika Baraza la Umoja wa
Mataifa. endelea …
Katika kikundi
chetu tunashughulikia na kujadili, Haki za Watoto na Agenda ya Mtoto na masuala
mbalimbali yanayowaguza watoto, tunakuwa na mada na kuijadili kwa siku hiyo.
Lakini vile vile kuelezea matukio mbalimbali ambayo yametukia kwa watoto kwa
muda wa wiki nzima.
Katika shughuli
zetu za mtandao wa wanahabari watoto, kwa kushirikiana na program ya kazi
tumeweza kutembelea maeneo mbalimbali ambayo yameweza kuathirika na mabadiiko
ya tabia ya nchi lakini na vile vile uchafuzi wa mazingira.
Katika maeneo
yale tumekuwa tunatembea na tunapiga
picha maeneo, tukisha piga picha tunawauliza wale watu wanaolizunguka lile eneo
na viongozi wao, tukimaliza tunaenda katika mitandao ya kijamii, kuna ramani,
ambapo watu wote duniani wanaweza kusoma kinachoendelea Tanzania na kuangalia.
Lakini vile
vile kipindi hicho hicho tunachoenda kupiga picha maeneo hayo, hicho kipindi
tunakitumia katika kurusha katika vipindi vyetu mbalimbali vya redio na TV
ambavyo tunavifanya mjini Mwanza na kuelimisha watu zaidi kuhusiana na
mabailiko ya tabia ya nchi na athari zake katika jamii inayozunguka.
Progamu hizo
tunazozifanya, ndizo zilizonifanya nikachaguliwa kwenda kuwakilisha vijana na
watoto Dunia nzima kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi, na kuhutubia Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa kuhusiana na vijana wananguvu ya kusimama na kuelezea kuhusiana
na mambo ambayo yanawakumba, kuhusiana na mabadiliko ya tabia ya nchi, na pia
wanao uwezo wa kusimama na kuchukua hatua kuhusiana na vitu vinavyowakabili,
hususan kuhusiana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Niliweza kueleza
viongozi kuwa wanatakiwa wakisha saini mkataba wa kazi kitu kinachofuata ni
kuchukua hatua siyo kusubiri mpaka matokeo makubwa kabisa yametokea ndio
wanachukua hatua. Wanatakiwa kuchukua hatua kuanzia sasa hivi ili kuweza
kutokomeza kabisa athari za tabia ya nchi kama tunavyozifahamu.
Athari kubwa
kabisa zinawakumba watoto zaidi katika jamii. Ukisikia ukame na mafuriko katika
vyombo vya habari watoto ndio wanaoathirika zaidi. Ndio maana niliweza
kuwashawishi wale viongozi kuwa wakisha saini ule mkataba wasisubiri muda mrefu
kutekeleza, wachukue hatua pale pale njia madhubuti za kupanaga kuepukana na
mabadiliko ya tabia ya nchi katika jamii.
|
0 comments:
Post a Comment