WIZARA YA AFYA,
MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA YA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KULAANI
MAUAJI YA WAZEE KATIKA WILAYA YA NZEGA, MKOANI TABORA:
KIPINDI CHA JANUARI - MACHI, 2016
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imesikitishwa na kulani viakli
matukio ya mauaji ya wazee kumi (10) yaliyotokea
wilaya ya Nzega, mkoani Tabora kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi, 2016.
Inaelezwa
kuwa, miongoni mwa chanzo cha mauaji ya wazee ni imani
za kishirikina, uchu wa kumiliki mashamba na visasi mambo ambayo Serikali
imekuwa ikiyakemea vikali. Wizara inawataka
wananchi kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Nzega, kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa mauaji haya wanakamatwa na kuchukuliwa hatua
kali ili kuwa fundisho kwa watu wengine.
Wizara inasisitiza kwamba wazee ni binadamu, na wanayo haki ya kuishi na
kupata hifadhi ya maisha yao kwa mujibu wa Sheria za nchi. Vitendo vya mauaji ya kikatili wanavyofanyiwa wazee vinasababisha hofu
kubwa kwa wananchi. Mauaji hayo yanawakosesha amani na vinadhohofisha ari ya kufanya
shughuli za za maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla. Familia inayoishi na mzee
anayewindwa, itatumia muda mwingi kutekeleza jukumu la ulinzi na hivyo kupunuza
tija na uzalishaji wa mwananchi mmoja na familia kawa ujumla. Kwa kutambua hili
Wizara inahimiza wadau wote kuunga mkono jitihada za Serikali katika ulinzi wa wazee
na kuboresha huduma zao ili kuelekeza nguvukazi katika uzalishaji.
Wizara inapenda kutoa pole kwa familia ambazo
zimeguswa na mauaji ya wazee waliopoteza maisha kwa kuuawa kinyama. Wizara inaitaka jamii itambue kuwa wazee wana haki ya kuthaminiwa utu wao,
kupata huduma stahiki, na kushiriki haki zote za msingi bila ubaguzi wowote
ambao unaweza kuhatarisha maisha yao ikiwemo haki yao ya kuishi. Aidha, Jamii
ihakikishe kuwa wazee na wananchi wote, wanaishi katika hali ya usalama, amani na
utulivu kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa letu.
Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
15/4/2016
0 comments:
Post a Comment