WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,
WAZEE NA WATOTO
(TAARIFA
KWA UMMA)
Taarifa inatolewa kwa umma
kwamba Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao chake cha
38 kilichofanyika tarehe 27 Januari, 2016 iliazimia kufuta usajili wa Shirika
la Kuleana Centre for Children’s Rights
kutokana na kukiuka masharti ya Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 (kama
ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005). Kwa tangazo la taarifa hii, shughuli za
Shirika tajwa zimekoma kuanzia tarehe ya taarifa hii. Wanachama wa shirika
wanaagizwa kufunga shughuli za shirika na kuzingatia taratibu za ufungaji wa
shughuli za Shirika kama zinavyoainishwa katika katiba ya Shirika na Kanuni za Sheria
ya NGOs, GN.Na.8 ya Mwaka 2015.
M.S.Katemba
MSAJILI
WA NGOs
2
Februari, 2016
0 comments:
Post a Comment