JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,
WAZEE NA WATOTO
(PRESS RELEASE)
WIZARA YAAGIZA KUKAMATAWA KWA WALIOMWOZESHA MTOTO WA MIAKA 13
WILAYA YA KISHAPU, MKOA WA SHINYANGA
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kwa masikitiko
makubwa na inataka hatua kali zichukuliwe dhidi ya wazazi wawili tofauti wanaotuhumiwa
kuwaozesha watoto wao wa umri wa miaka 13 na kuwakatisha masomo katika mkoa wa
Shinyanga na Dodoma
Imeelezwa
kuwa, wakati mtoto mmoja mwanafunzi wa shule ya msingi Wishiteleja wilayani
Kishapu mkoa wa Shinyanga ameozeshwa kwa nguvu kwa mahari ya ngombe 13 na
kumkatisha masomo yake akiwa darasa la sita, mtoto mwingine wa mtaa wa Chikole,
Kata ya Msalato Manispaa ya Dodoma anasemekana kuozeshwa kwa mahali ya shilingi
600,000. Kufuatia kuwepo kwa matukio haya mawili Wizara inataka vyombo vya dola
kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi wa Mtoto katika mikoa yote kuhakikisha
kuwa watuhumiwa wanachukuliwa hatua kali.
Tukio
la kuwaoza watoto katika umri mdogo siyo tu linakinzana na haki za msingi za mtoto
bali pia linamkosesha mtoto haki ya kuendelezwa ikiwa ni pamoja na kuhatarisha uhai
wake kwa kupatiwa majukumu ya mtu mzima katika umri mdogo.
Wizara
inawataka wazazi na walezi kubadilika na kuachana na tabia ya kuwaoza watoto wao
katika umri mdogo maana vitendo hivyo ni vya kikatili. Jamii inatakiwa kutambua
kuwa, vitendo vya kikatili kama hivyo
vinapofanywa katika familia vinarudisha nyuma juhudi za Serikali za kupambana
na ukatili maana kwa kiasi kikubwa familia inatakiwa kuwa mahala salama
panapofaa watoto kuishi na kulindwa.
Aidha,
Wizara inakumbusha wazazi,
walezi na wadau wengine kuwa, ndoa za utotoni ni kinyume na Sheria ya Mtoto
(2009) na Mikataba ya Kimataifa kuhusu Haki na Ustawi wa Mtoto. NIwajibu wa
kila mtu kuhakikisha kuwa watoto wanaishi katika usalama na kuhakikishiwa
haki zao zote za msingi ikiwemo
kulindwa, kuendelezwa, kuishi na
kushirikishwa katika maisha ya kila siku ili kujenga Taifa linaloheshimu maslahi
ya watoto.
Erasto T.
Ching’oro
Kny: KATIBU MKUU
MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZAZI NA WATOTO
0 comments:
Post a Comment