TAARIFA KWA UMMA
KUSUDIO LA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MASHIRIKA YASIYO YA
KISERIKALI YANAYOJIENDESHA KINYUME CHA SHERIA
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali anakusudia kuyachukulia hatua Mashirika yanayoendesha shughuli zao
kinyume cha Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka
2005. Mashirika hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa
kipindi cha miaka miwili pasipo kutoa sababu za msingi, kulipa ada ya mwaka au
kuendesha shughuli za NGOs bila kusajiliwa chini ya Sheria ya NGOs.
Kwa taarifa hii, Mashirika husika
yanatakiwa yawe yamerekebisha dosari tajwa ndani ya siku thelathini (30)
kuanzia tarehe ya tangazo hili. Baada ya kipindi hicho, Msajili wa NGOs
atayafutia usajili Mashirika ambayo yatakuwa hayajawasilisha taarifa na
kuyachukulia hatua stahiki Mashirika yanayoendesha shughuli za NGOs bila ya
usajili chini ya Sheria husika.
Malipo yote ya ada yafanyike kupitia Benki ya NMB, NGO Account Na. 20110014074
na stakabadhi halali ya malipo itumwe kwa Msajili wa NGOs.
Imetolewa na,
MSAJILI WA NGOs
WIZARA
YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
06
Januari, 2016
0 comments:
Post a Comment