BODI INAUNDWA NA
NANI?
|
Bodi ya Taifa ya Uratibu wa NGOs ni chombo cha juu cha
usimamizi wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.Chombo hiki kimeundwa
kwa mujibu wa Sheriaya NGOs Na.24 ya mwaka 2002 Kifungu cha 6(1).Sheria hii
imeweka utaratibu wa kuanzisha vyombo vikuu viwili vya kitaifa, yaani Bodi ya
Taifa ya Uratibu wa NGOs (National NGOs Coordination Board) na Baraza la
Taifa la NGOs (National Council for Non Governmental Organizations)
|
Bodi ya Taifa ya Uratibu wa NGOs ilianza kazi yake
rasmi tarehe 20 Aprili 2004 kwa uzinduzi uliofanywa na aliyekuwa Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Kuondoa Umasikini na Uratibu wa NGOs, Mh.
Maokola Majogo.Aidha, katika mabadiliko ya Wizara yaliyofanyika kipindi cha Serikali
ya Awamu ya Nne, jukumu la kuratibu NGOs limewekwa chini ya Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuanzia mwezi Februari 2006.
|
DIRA YA BODI
|
Kuona Mashirika Yasiyo ya Kiserikali imara na kuhakikisha
kuwepo na mazingira bora mazuri yatakayowezesha NGOs kufanya kazi kwa ufanisi
zaidi, kuongeza ushirikiano na Serikali pamoja na wadau wengine na hivyo
kuchangia kikamilifu katika kupunguza umaskini na maendeleo ya Taifa kwa
ujumla.
|
UTUME WA BODI
(MISSION)
|
Utume wa Bodi ni kuratibu, kusimamia usajili wa NGOs na
kuwezesha uendeshaji wa shughuli za NGOs nchini kwa mujibu wa Sheria ya NGOs
kwa kushirikisha wadau wote.
|
UTEUZI WA
WAJUMBE WA BODI
|
Bodi ina jumla ya wajumbe kumi (10) kati ya hayo
Mwenyekiti huchaguliwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano baada ya kupokea
mapendekezo kutoka kwa Waziri anayesimamia mashirika yasiyo ya kiserikali.
|
Wajumbe wanne (4) huteuliwa na Waziri kwa mapendekezo
kutoka Baraza la Taifa la NGOs, wajumbe hawa huwakilisha sekta ya NGOs. Aidha
wajumbe wengine watano ( 5) huchaguliwa na Waziri kwa kuzingatia uzoefu wao
katika kulitumikia Taifa, hawa huwakilisha upande wa serikali. Kati ya
wjaumbe hawa watano (5) Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali (NGO's Coordination Department) huwa ndiye katibu wa Bodi
kwa wadhifa wake.
|
MAJUKUMU YA BODI
|
Kuidhinisha na kuratibu usajili wa mashirika yasiyo ya
kiserikali
kuwezesha utekelezaji wa sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo
ya Kiserikali ( NGOs)
Kuwezesha uratibu wa shughuli za mashirika yasiyo ya
Kiserikali ( NGOs)
Kuidhinisha maombi ya usajili au ya vyeti vya ukubalifu
Kutoa maelezo juu yai ya kusimamishwa au kufutiwa usajili
shirika lolote lisilo la kiserikali
Tathmini ya taarifa mwaka za utekelezaji wa shughuli
za mashirika yasiyo ya Kiserikali ( NGOs)
Kuishauri serikali kuhusiana na shughuli za mashirika
yasiyo ya kiserikali
Kupitia rejista ya mashirika yasiyo ya kiserikali.
kutoa miongozo ya kisera kwa mashirka yasiyo ya kiserkali
kwa ajili ya kuoanisha shughuli za mashiruika hayo na mpango wa Taifa wa
maendeleo.
Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa za kawaida za
baraza, na kutoa ushauri wa mkakati endelevu utakaowezesha usimamizi thabiti
wa shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali.
kuwezesha kuwepo kwa miundombinu na mitandao ya
upashanaji habari kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali na Serikali.
kuchunguza na kuhoji jambo lolote ili kuhakikisha Shirika
Lisilo la Kiserikali linazingatia katiba yake na kwa mujibu wa sheria.
kufanya shughuli yoyote kama itakavyoagizwa na waziri
muhisika.
|
VIKAO VYA BODI NA UTEKELEZAJI
WA MAJUKUMU
|
Kisheria Bodi ya Taifa ya Uratibu wa NGOs inatakiwa
kukutana mara moja kila baada ya miezi mitatu.Hata hivyo inaweza kufanya
kikao cha dharura wakati wowote ikibidi. Ili kuweza kutekeleza majukumu yake
kwa ufanisi, Bodi imekasimu baadhi ya majukumu yake kwa Sekretarieti yaani
Idara ya Uratibu wa Shughuli za NGOs. Utekelezaji wa majukumu haya
unasimamiwa na Mkurugenzi wa NGOs ambaye ndiye Katibu wa Bodi kisheria. Hii
ni kwa mujibu wa Kifungu cha 2 (b) cha Sheria ya NGOs Na.24 ya mwaka 2002
|
Wednesday, 11 November 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment