JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
TARATIBU
ZA USAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
(KWA
MUJIBU WA SHERIA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI NA. 24, 2002)
1.0 TARATIBU ZA USAJILI
Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
unaofanyika chini ya sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Na. 24 ya mwaka
2002 umegawanywa katika ngazi nne kama ifuatavyo;
1.1 Ngazi
ya Wilaya
1.2 Ngazi
ya Mkoa
1.3 Ngazi
ya Taifa
1.4 Ngazi
ya Kimataifa
Msajili
wa Mashirika ya kiserikali amepewa mamlaka chini ya kifungu cha 22(1) cha
sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24, ya mwaka 2002 kuteua maafisa
wa umma katika wilaya au mkoa kwa ajili ya kuwezesha usajili katika ngazi
husika. Katika mfumo uliopo sasa maafisa wa umma wanaotajwa katika sheria ni
Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya na Mkoa ambao kwa namna nyingine huitwa
wasajili wasaidizi.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 12(1) cha sheria, maombi ya usajili yatawasilishwa na
kikundi cha watu kwa Msajili kupitia fomu maalumu (NGO A Fomu Na. 1). Maneno
“kikundi cha watu” yanahusisha kikundi cha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Hata
hivyo, kanuni ya 3 ya Kanuni za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali zilizofanyiwa
marekebisho mwaka 2015 kupitia tangazo la serikali Na. 8 inaweka sharti la
kikundi kuwa na watu/wanachama wasiopungua watano.
Kulingana na kifungu cha 12(2) cha Sheria ya
NGOs Na. 24/2002, Maombi
ya usajili wa NGOs yanatakiwa kuwa na viambatanisho vifuatavyo:-
a) Katiba
ya Shirika lisilo la Kiserikali (Nakala 3 zilizojaladiwa - Bound)
b) Maelezo
binafsi (Wasifu) wa viongozi 3 (CV) na picha 2 kwa kila CV - (Mwenyekiti,
Katibu na Mhazini, au wengineo kulingana na mahitaji ya Shirika)
Angalizo: kwa NGOs za
kimataifa - CV mbili ziwe za raia wa Tanzania.
c) Muhtasari
wa kikao cha kuanzishwa kwa Shirika ukiambatanishwa na majina na saini za
wanachama waanzilishi.
d) Fomu
ya maombi ya usajili (NGO A Form No. 1) iliyojazwa
na mwombaji/waombaji na kubandikwa ushuru wa stempu za shilingi 1,500/= au USD 2 kwa NGOs za Kimataifa.
e) Barua
ya Utambulisho kutoka kwa Msajili Msaidizi (Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa,
Halmashauri /Manispaa/ Wilaya).
f) Maelezo
yoyote au taarifa kama itakavyohitajiwa na Msajili.
2.0 ADA
ZA USAJILI
a) Ngazi
ya Wilaya - Shs 80,000/=
b) Ngazi
ya Mkoa - Shs 100,000/=
c) Ngazi
ya Taifa - Shs 115,000/=
d) Ngazi
ya Kimataifa - Dola za kimarekani
350
Maombi yatumwe kwa;
Msajili
wa NGOs,
Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
8
Barabara ya Kivukoni
S.L.P
3448
11486 DAR ES SALAAM.
Simu 213526/2137679/2123146
Tovuti -http//www.tnnc.go.tz
nina swali je nataka kusajiri NGO ya Kitaifa je natakiwa kuanzia ngazi gani mpaka kufikia kusajiri Kitaifa?
ReplyDeleteNaomba niambiwe fomu ya usajili inapatikana wapi kwani kwenye tovuti haipo labda kama nimekosea mahali pa kuipata,enviculture@gmail.com
ReplyDeleteKuna tofauti kati ya shirika na Taasisi?
ReplyDeleteKuna tofauti kati ya shirika na Taasisi?
ReplyDelete