WIZARA YA AFYA, MEANDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA
WATOTO.
TAARIFA
KWA UMMA
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali anatarajia kuhakiki Mashirika yote Yasiyo ya Kiserikali kuanzia tarehe
21 hadi 31 Agosti, 2017. Lengo kuu la zoezi hili ni Kuhuisha orodha ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali nchini, Kuboresha Kanzi Data ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
na kupima utekelezaji wa majukumu ya Mashirika haya. Zoezi hili litafanyika katika
Kanda tano (5). Kanda ya Mashariki itahudumia mikoa ya DAR ES SALAAM, LINDI,
MTWARA, PWANI na MOROGORO na Kituo kitakuwa Idara ya Uratibu wa NGOs DAR ES SALAAM; Kanda ya Kati itahudumia mikoa ya DODOMA,
SINGIDA, TABORA na KIGOMA na Kituo kitakuwa DODOMA, Makao Makuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto iliyopo Chuo Kikuu cha Dodoma,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii, Jengo Na. 11, Dodoma;
Kanda ya Kaskazini itahudumia mikoa ya KILIMANJARO, TANGA, ARUSHA na MANYARA na
Kituo kitakuwa katika Ofisi ya Katibu Tawala (M) KILIMANJARO; Kanda ya Ziwa itahudumia mikoa ya MWANZA, KAGERA,
MARA, GEITA, SIMIYU na SHINYANGA na Kituo kitakuwa katika Ofisi ya Katibu
Tawala (M) MWANZA na Kanda ya Nyanda
za Juu - Kusini itahudumia mikoa ya MBEYA, RUVUMA, KATAVI, RUKWA, SONGWE,
NJOMBE na IRINGA na Kituo kitakuwa katika Ofisi ya Katibu Tawala (M), MBEYA.
Wakati wa uhakiki kila shirika
linapaswa kuwasilisha Cheti Halisi cha Usajili, Nakala ya Cheti cha Usajili,
kujaza fomu ya uhakiki NGO-Fomu/UHK/2017
inayopatikana katika Tovuti (www.tnnc.go.tz), Stakabadhi
za Malipo ya Ada ya mwaka toka kuanzishwa kwa shirika, Barua kutoka kwa Afisa Maendeleo
ya Jamii (Mkoa/Wilaya/Halmashauri/Manispaa) ikithibitisha uwepo wa Ofisi ya Shirika
na nakala ya katiba iliyothibitishwa na Msajili wa NGOs. Aidha, Mashirika yote yatakayoshindwa
kuhakikiwa katika vituo vya Kanda tajwa hapo juu, yatafutiwa Usajili na kuondolewa
kwenye Regista ya Msajili wa NGOs. Ili kutoa fursa ya kuhuisha Kanzi Data na Benki
ya Takwimu, Usajili wa NGOs utasitishwa kuanzia tarehe 21 Agosti hadi 30
Novemba, 2017.
M.S. Katemba
MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI